Hili ni somo linalohusu namna mwanadamu anavyotakiwa kufanya ili aweze kumshinda Ibilisi, mchakato huu wa kumshinda Ibilisi ni mkubwa na mgumu ambao huhusisha sehemu zote za mwili yaani roho, nafsi na mwili. Roho ndiyo sehemu ya mwili ambayo huhitaji kujazwa nguvu ya Mungu ili iweze kuushinda mwili ambao ni wa dunia hii, mwili ambao nia yake ni uharibifu kama tutakavyoona katika somo hili.
Mwanadamu anakuwa na roho ambayo huwa kama imezimia au haifanyi kazi ipasavyo pale ambapo anakuwa ameshikwa na maovu na kutokumtumikia Mungu, wakati huu roho hii hujazwa na roho chafu ambazo haziendani na mapenzi ya Mungu kwa maana hazitokani na Mungu. Akisha kumpokea Yesu mtu huyu hujiwa na Roho Mtakatifu ambaye kwa kutegemea na jinsi huyu mtu anavyojiweka karibu na Mungu ndivyo huendelea kukua na kujijenga, mtu huyu huanza kumshinda shetani na kuuzuia mwili wake kutenda dhambi.
Karibu katika sehemu ya pili ya somo hili, tutazame pamoja mambo ambayo husaidia kuijengea mazingira roho yako kukua.
Vyakula vya kiroho ni hivi vifuatavyo:
1. Maombi
2. Neno la Mungu
3. Nyimbo za kumsifu na kumtukuza Mungu
4. Tafakari na mawazo juu ya Mungu na matendo yake makuu.
Mambo ambayo husaidia kuijengea mazingira roho yako kukua
Kuna mambo katika maisha ambayo kwa kawaida mwanadamu anayafanya, lakini nikufahamishe leo kuwa katika mambo yote unayoyafanya yana athari katika ulimwengu wa roho na makuzi ya roho yako yanategemea moja kwa moja mambo hayo, hebu sasa tuangalie baadhi ya mambo ambayo yanaweza kukusaidia kuikuza roho yako.
1. Vitu unavyopenda kuangalia.
Zaburi 119:37
“Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa, unihuishe katika njia yako.”

Kuna vitu ambavyo havifai kama Daudi anavyosema ambavyo vitajaa ndani ya nafsi yako kama ukiendelea kuviangalia, picha za uchi, matendo ya kikatili na matusi. Kimsingi vitu ambavyo havikupi kuongezeka kimaarifa na wala haviisaidii roho yako kukua siyo vizuri kuviangalia.
Mtu mmoja kaniuliza swali, “Kwani kuna maasi gani kwa mimi kuangalia mziki wa bongo flava?” na mimi nikamuuliza, kwani napata nini cha zaidi ambacho ni cha faida kwa kuangalia hayo? Kimsingi vitu hivi, kabla hatujazama ndani zaidi vinatumiwa tu kumsahaulisha mtu majukumu yake na kumchelewesha. Suala siyo kupata burudani, kwani Mungu hutuburudisha na ziko burudani nyingi zenye utukufu wa Mungu ambazo tunaweza kuzitumia badala ya kila saa kukubali kuburudishwa na watu ambao hawana hofu au imani tuliyonayo sisi.

Vipo vitu vya msingi ambavyo waweza kuviangalia na visikudhuru, lakini uwe makini kuna wakati baadhi ya vitu vinaweza kuwa havina athari ya moja kwa moja katika maisha yako ya kiroho lakini vikakuchukulia muda wako mwingi sana kuliko muda wa kusoma neno la Mungu na kuomba.
Vitu hivyo ni kama muvi na mpira na vilevile kucheza gemu. Ni kweli kwamba kuna wakati ambao mtu huhitaji kupumzika na kujiburudisha kidogo baada ya kazi, wala hapa sikusudii kuwapiga marufuku watu kufanya vitu hivi, lengo langu hapa ni kukutahadharisha tu kuwa kama ambavyo vitu hivi vinaweza kukuchelewesha kupika na kusababisha ukaahirisha kula chakula cha kimwili, vilevile vinaweza kukuharibia ratiba yako ya kuilisha roho yako. Hivyo unapoviangalia hivi hakikisha kuwa haviathiri ratiba yako ya kwenye maombi wala ya kusoma biblia.
Anaposema Daudi kwamba anaomba kuhuishwa katika njia ya Mungu anamaanisha nini? Anataka kujizoeza kuviangalia vitu ambavyo vitamkuza katika maisha yake ya rohoni. Angalia sana ni vitu gani unavyovitilia maanani katika maisha yako ili usije ukapotea.
2. Vitu unavyovisikiliza mara kwa mara
2korintho15:33.
“Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.”
Kile unachopenda kukisikiliza kama ni kibaya, katika mazungumzo na rafiki zako, tabia yako itaendana na yale mazungumzo. Nakumbuka nikiwa mdogo nilichelewa sana kuzifahamu habari za mapenzi na wasichana kwa sababu rafiki zangu walikuwa hawaziongelei kabisa, ulipofika muda wa kubalehe mimi nilikuwa nina tabia ya kujitenga na kila aliyekuwa anapenda habari hizo, nikawa na tabia njema lakini baadaye nilipopata marafiki wapya ambao walikuwa wanapenda sana habari hizo, nilijikuta naharibikiwa na kuingia kwenye tabia hiyo mbaya kama nini sijui!
Ndiyo maana wapendwa wenye watoto mnapaswa kuwaangalia sana kuhusu marafiki gani wanaokuwa nao muda mwingi, yumkini mzazi wangu angekuwa makini katika hilo angeniondoa pale nilipokuwa nimetumbukia enzi hizo. Lakini simlaumu, kwa kuwa hakujua.
3. Vitu unavyopenda kuviongea mara kwa mara.
Zaburi 141:3
“Ee Bwana, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.”
Daudi anamuomba Mungu aweke mngojezi mlangoni pa midomo yake ili aweze kuongea mambo yenye utukufu mbele za Mungu. Kile unachokisema mtumishi wa Mungu kinasaidia sana katika kuamua kwamba wewe ni mtu wa Mungu na kukutambulisha kwa wengine kama umeokoka kweli, basi kama mtumishi wa Mungu unapenda kunena maneno machafu yanayopelekea watu wengine kuumia utasababisha magomvi na kujikosesha amani hali ambayo itasababisha ushindwe kusoma neno wala kuomba kwa sababu moyo wako saa zote umekwazika na hauna amani.
Marko 7:20
“Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.”
Ni afadhali unaposikia maneno yanayokukwaza ukanyamaza kuliko kuongea katika hasira kwani maneno unayoyatoa yanaweza kuzidisha magomvi.
Biblia imetoa maonyo mengi sana kuhusu maneno na kumuhimiza mtu wa Mungu kuwa na maneno machache, awe mwepesi wa kusikia lakini asiwe mwepesi wa kuongea, mahali hapa pasingetosha kujadili athari za ulimi kwani ni mambo mengi sana yanayohusiana nao ambayo tungepaswa kuyapitia. Cha msingi hapa tu ni kuwa makini na kumuomba Mungu ili yale tunayoyasema na kuwaambia watu yawe yamekolea munyu, yaonye, yafundishe, yatie moyo na kuendeleza upendo na msamaha.
Wakolosai 4:6
“Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.”
4. Vitu vilivyo moyoni mwako.
Zaburi 119:11
Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.
Daudi ana kitu alichokiweka ndani ya moyo wake ambacho kinamsaidia kuishi sawasawa na mapenzi ya Mungu, kwanini Daudi ameliweka neno la Mungu moyoni, na siyo mahali pengine? Ni kwa sababu moyo ndiyo huwa chanzo cha uzima na chanzo cha mauti, kilicho moyoni ndicho hutoka moja kwa moja na kuathiri maisha ya mtu.
Jeremiah 17:9
Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?

Hapa tunaonywa kuhusu tabia za moyo.
Luka 6:45
Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.
Moyoni hujaa vitu ambavyo ndivyo huwa vinaamua au vinaonesha mshindi kati ya mwili na Roho wa Mungu, kama Roho wa Mungu akikaa kwa wingi ndani yako, moyo wako huwa ni ghala yake ya kuhifadhia mambo mema, humo huwekwa silaha na chakula cha kuendelea kuiimarisha roho yako na kuudhoofisha mwili, lakini vivyo hivyo kinyume chake, Mwili ukishinda basi huutawala mwili na roho yako na kuweka chakula cha hizo roho chafu na kila aina ya kazi za uasi ndani ya moyo, ni katika hali kama hiyo ambapo mwandishi anaandika hapa kuwa usiuache moyo bila kuujaza mambo mema maana huwa unakuwa mdanganyifu sana katika mambo yake.
Kile kitakachoujaza moyo wako ndicho kitakachokupa ushindi katika maisha unayotaka kuyaishi ikiwa hasa ni ya rohoni, ukiujaza moyo wako masengenyo wewe utakuwa ni wa masengenyo tu, ukiujaza tamaa wewe utakuwa ni wa tamaa tu. Ndiyo maana Daudi alisema kuwa moyoni mwangu nimeliweka neno lako ili nisikutende dhambi ambapo akiisha kuliweka neno la Mungu ndani yake kwa wingi, badala ya kuwa na mambo mengine mabaya ndani yake anakuwa na maneno ya uzima yanayomuelekeza kutenda mema na kumuishia Mungu siku zote.

Mithali 4:23
Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Tunaonywa hapa kuwa moyoni ndiko kutokako chemchemi za uzima, utakachoweka moyoni mwako ndicho hasa kitakachoamua kama wewe ni wa uzima au ni wa mauti, chunga sana ukiwekacho moyoni, ama hakika moyo ni kama ikulu ya Mungu, ndiyo makao makuu ya Mungu pindi ajapo ndani yako.
Roho huwa ni mapokezi ya yule Mungu anayetakiwa kuabudiwa na akiisha kupokewa, mambo yake na matendo yake na mwongozo wake huenda kuhifadhiwa moyoni na ni kutoka pale moyoni ndipo mambo hayo huchukuliwa na kuwekwa kwenye matendo.
Kwa mfano, roho wa uzinzi humuingia mtu, akiisha kumuingia huweka mawazo mabaya katika moyo wa huyu mtu na huyu mtu huanza kuwaza uzinzi, akiisha kuiva katika hayo mawazo, moyo wake ukiisha kujazwa mawazo mabaya, basi huyu mtu atakachoongea, atakachofanya na atakachofikiria itakuwa ni uzinzi tu, maneno yote yatakuwa yanaendana na uzinzi na matendo yote hata yasiyofungamana na uzinzi atayapeleka kwenye uzinzi.
Ndiyo maana mawazo ya watu walio wengi huwa yanapeleka maongezi mengi kwenye uzinzi, akimuona msichana mawazo yake yanapita na yule msichana kwenye uzinzi kwanza kabla ya kuanza kuwaza mambo mengine, hiyo ni tofauti na mtakatifu anavyotakiwa kuwaza, maana siku zote kila nikimuona mtu natakiwa kuwaza kwanza kabla ya yote kama amempokea Kristo au la, na kama la nitafanyaje ili ampokee, haleluya!
Moyo, ndiyo sehemu ya mwanadamu inayotafutwa na hizi serikali mbili: Mungu na Ibilisi, Mungu asingejivunia Ayubu kama moyo wa Ayubu ungekuwa mbali naye, au ungekuwa unahifadhi vitu tofauti na Mungu. Mungu hakuwa anajivuna kwa jinsi alivyombariki Ayubu, hakujivunia utajiri wa Ayubu, hakujivunia umaarufu wake isipokuwa alijivunia unyofu wa moyo wake! Tazama anavyosema

Ayubu 1:8
Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.

Hoja kubwa anayojivunia Mungu juu ya Ayubu siyo mali, bali ni unyofu na unyenyekevu wa Ayubu ambaye alikuwa ana “mcha Mungu na kuepukana na uovu.” Ukiangalia swala hili ndilo alilolisema Daudi likiwa ndilo lengo hasa la kuliweka neno la Mungu kwa wingi ndani yake- “nisije nikakutenda dhambi” kwa hiyo tunajiridhisha kuwa moyo wa Ayubu ulijaa utakatifu na mawazo mema ya Mungu na neno lake; ndiyo maana hata shetani aliporuhusiwa kupiga vitu vyote vya Ayubu, bado Ayubu alibaki kuwa mwaminifu kwa Mungu wake kwani moyo wake ulikuwa umeambatana na Mungu na siyo na vitu.
Angalia sana moyo wako umeambatana na vitu gani, maana kwa kila unayemtumikia kati ya Mungu au shetani, moyo ndiyo unatakiwa kuwa makao makuu na hazina kuu ya ufalme husika; Mungu aliwachukia waisraeli siyo kwa kutokwenda kanisani, bali alisema ingawa wanakuja kanisani na kunitolea sadaka, siwakubali kwani hawa hunikubali kwa vinywa vyao tu lakini mioyo yao iko mbali nami.

Isaiah 29:13-14
“Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walicho nacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa; kwa sababu hiyo mimi nitafanya tena kazi ya ajabu kati ya watu hawa, kazi ya ajabu na mwujiza; na akili za watu wao wenye akili zitapotea, na ufahamu wa wenye busara wao utafichwa.”
Unaona hapa? Mungu hagombani na watu kwa sababu hawamkaribii, bali wanamkaribia huku mioyo yao iko mbali nao! Kwa hivyo moyo ni ikulu, Mungu akitaka kumtawala mwanadamu anamtaka mwanadamu ampe moyo wake ili apate uhalali wa kuyaongoza maisha ya mtu huyo, na shetani vilevile atapata uhalali wa kuyakalia maisha yako ikiwa utampa moyo wako.
Maisha ya mtu na Mungu yanafananishwa na maisha ya mtu na mpenzi wake, au maisha ya Kristo na Kanisa yanafananishwa na maisha ya mtu na mwenzi wake. Mtu akimpenda mwenzi wake humpa moyo wake na mtu kama huyo yuko tayari kufanya lolote ili tu asimpoteze mwenzi wake, ni hatari kama mtu huyo akiwa amempa mwenzi wake moyo halafu yeye hajachukua moyo wa mwenzie, ndipo unapokutana na mapenzi ya kulia kila siku kwani mwanaume huyu aliyempa binti yule moyo masikini anajitahidi kufanya kila kitu ili msichana yule ampende lakini wapi! Ndiyo maana watu hufikia hata maamuzi ya kujinyonga kwa sababu kiukweli amekabidhi moyo kwa mwenziwe kwa hiyo yule mwenzi anamuendesha kama anavyotaka maana anakuwa anajua kuwa moyo wako anao sasa anautumia kukuendesha kama mtu abadilishavyo chaneli kwenye televisheni!
Usitoe moyo wako kwa watu ambao hawako tayari kukupa mioyo yao, utaumia! Acha Mungu akuongoze na umpe moyo wako ili uwe salama milele na akuponye na kukuongoza usikutane na waibao mioyo ya watu bila kutoa ya kwao. Kwenye mahusiano tunatakiwa kubadilishana mioyo siyo mmoja achukue moyo wa mwenzie halafu wa kwake abaki nao, ni hatariii!
Pole wewe uliyekumbwa na hayo, nenda mbele za Mungu umuombe akurudishie moyo wako ulioibiwa! Subiri nikwambie kitu, kwenye mahusiano ni mioyo tu ndiyo inayohusika, sasa utakuta mtumishi kabla ya kuwa na mwenzi alikuwa saa zote anatafakari neno sasa tangu amempata yule shemeji yangu, sweet heart, amemjaza moyoni hata nafasi ya kuimba pambio na kusoma biblia hana, akienda huku anamuwaza yeye, akirudi kwa rafiki zake anamuongelea yeye, akipiga simu anaongea na yeye, akiandika meseji anamuandikia yeye, akilia anamlilia yeye, akinunua zawadi anamnunulia yeye, akicheka kachekeshwa na yeye, akilia kalizwa na yeye, akiumia hapoi hadi apewe pole na yeye, akilizwa na mwingine hanyamazi hadi anyamazishwe na yeye. Akikatazwa jambo haachi mpaka akatazwe na yeye! Kwenda kanisani mpaka asukumwe au asindikizwe na yeye! Sasa mtu kama huyu akiachwa kwanini asinywe sumu jamani?
Sasa unajiuliza hapa nataka kusema nini, nasema uwe na kiasi na kukesha-naye Bwana atakupa taji ya uzima. Mwenye masikio ya kusikia na asikie.
Unasikia wewe kijana, hatujaanza leo kuwa na wapenzi na wala sisemi kuwa kuwa na wapenzi ni vibaya la! Ninachosema ni kuwa kuutiisha mwili ni pamoja na kuupunguzia na kuudhibiti pale ambapo unaonekana kuvuka mipaka, kwani unafikiri kwanini watu wanazini na ndugu zao? Ni kwasababu mwili usipodhibitiwa huendelea mbele na kufanya mambo yasiyofaa na hivyo mwenye mwili asipouzuia, mwishowe atafanana na Ibilisi.
Unataka kumpendeza Mungu, basi funga, omba, jitakase soma neno, sasa wewe unayeshinda na mwenzi wako hayo utayafanya saa ngapi? Watu kama wewe ndo wale ambao wakiisha kuoana wanataka wawe wanashinda ndani na wapenzi wao wakitazamana na kucheza usiku kucha, huwa hawakawii kushinda njaa! Muache mumeo amtafute Mungu! Muache mchumba wako amtafute Mungu! Muache sweetheart wako amtafute Mungu! Mkaripie pindi anapoonesha udhaifu katika kumtafuta Mungu! Au unataka kuingia mbinguni peke yako? Haaaaaaaaah!
Tunapoongelea kwa mfano suala la kufunga, hatusemi chakula hakina maana, chakula ni afya lakini tunalazimika kufunga ili kuiadabisha miili yetu mbele ya Mungu, hatusubiri miili kupoteza hamu ya kula ili tufunge, tena siku nzuri ya kufunga ni ile unayojisikia kula na una njaa tangu saa kumi na moja alfajiri! Unajua nikushirikishe jambo hapa, nimewahi kufundisha watu kuhusu sadaka, kwa kusema kuwa unapomtolea Mungu sadaka usitoe cha ziada bali kile ambacho kinauma.
Mungu wetu siyo Mungu wa mabaki bali Mungu wa kilicho bora! Ndiyo maana hata wewe umechagua mchumba mzuri kweli! Unaona ee? Yaani katika ufalme wako (katika mbingu yako) hutaki kinyonge kiingie! Na vilevile Mungu anataka the best! Kilicho bora kabisa! Sasa huyu kwa vile alivimbiwa jana akateseka sana anataka afunge leo maana hana ‘mudi’ ya kula, looh! Aibu!
Tunafanya vitu hata tusivyojisikia kufanya kwa ajili ya Bwana kwa sababu sisi tu watumishi wake, hata tukiwa wana tunatakiwa kufuata mfano wa Kristo maana anasema mimi sikusema wala kufanya jambo lolote lile isipokuwa nililoagizwa na baba, pale Getsemane unaona Yesu anasema mapenzi yako baba yatimizwe, ina maana yeye anajisikia kutoendelea kama wewe leo unavyoweza kujisikia kuacha kusudi la Mungu. Lakini hebu tiwa nguvu na umwambie Mungu ili mapenzi yake katika maisha yako yatendeke kwa jina la Yesu!

No comments:
Post a Comment