Showing posts with label Habari katika injili. Show all posts
Showing posts with label Habari katika injili. Show all posts
Tuesday, February 14, 2017
FIMBO YA MUSA GOSPEL ARTISTS
MJUE BENJAMIN DUBE
Mziki wa Afrika ya kusini ni muziki maarufu tangu kitambo.
Ni mziki ambao unafahamika kwa uzuri wa melodi na tyuni zenye hisia kali sana.
Kwa upande wa muziki wa injili, Afrika Kusini
imeendelea kutajwa kama nchi yenye vipaji vingi vikubwa sana.
Msanii ambaye tutamuongelea leo anaitwa Benjamin Dube. Yeye ni
msanii mkubwa sana katika tasnia ya muziki wa injili wa Afrika ya kusini. Uzuri
wa mashairi yake; uzuri wa nyimbo zake pamoja na nguvu ya Mungu inayopatikana katika
nyimbo zake inamfanya apendwe sana.
Si hivyo tu bali Benjamini Dube anafahamika
kwa unyenyekevu wake. Yeye siku zote anasema ‘in gospel we don’t have who is who,
who is better than the other… but in gospel we complement each other” yaani katika
mziki wainjili hatuna nani ni nani, yupi ni bora kuliko mwingine… bali katika mziki
wa injili tunakamilishana.
Anafahamika kwa juhudi na kujitoa kwake katika huduma; kwani
kwa mwaka anashiriki katika matoleo mawili. Anatoa toleo la kwake; anatoa toleo
la Spirit of praise na anashiriki katika kuwasaidia wasanii wenzake katika matoleo
yao.
Zipo nyimbo kadhaa ambazo zinaimbwa hapa Tanzania ambazo ziliimbwa
naye kwa mara ya kwanza
Nazo ninakupenda eeYesu; Amen, na hakuna wa kufanana namwokozi
wangu/nimemwona anapendeza.
Sunday, February 12, 2017
MARTHA BARAKA: Unyenyekevu na kujishusha ni muhimu
Msanii wa nyimbo za injili Martha Baraka amewataka wasanii na
watu maarufu kuwa wanyenyekevu ili waweze
kuishi na watu vizuri na hata kudumisha ndoa zao.
Martha Baraka amesema licha ya kuwa yeye mwenyewe anatetemekewa
sana na watu na kukatiwa hata tiketi za ndege anapokuwa kwenye ziara za huduma;
bado akifika nyumbani anauacha ule u Martha Baraka wake mlangoni na kuendelea kumhudumia
mumewe kama mke.
“Nimetoka Mwanza, watu walikuwa wananitetemekea na wakanikatia
tiketi za ndege… lakini nikifika nyumbani, ule u – Martha Baraka na umaarufu wangu
inabidi uishie mlangoni”
Akiongea na mwanahabari wetu Yona David; Martha Baraka
alionekana kumaanisha anachokisema na alikuwa na nasaha za muhimu sana kwa wasanii
na waimbaji maarufu ambapo alikiri kuwa yeye kama yeye anajitahidi sana kuwa
mama anapokuwa nyumbani na anamnyenyekea mume wake bila kujali kwamba jina lake
ni kubwa sana kwenye jamii.
Subscribe to:
Posts (Atom)







