Sunday, February 12, 2017

MARTHA BARAKA: Unyenyekevu na kujishusha ni muhimu

Msanii wa nyimbo za injili Martha Baraka amewataka wasanii na watu maarufu kuwa wanyenyekevu  ili waweze kuishi na watu vizuri na hata kudumisha ndoa zao.

Martha Baraka amesema licha ya kuwa yeye mwenyewe anatetemekewa sana na watu na kukatiwa hata tiketi za ndege anapokuwa kwenye ziara za huduma; bado akifika nyumbani anauacha ule u Martha Baraka wake mlangoni na kuendelea kumhudumia mumewe kama mke.

“Nimetoka Mwanza, watu walikuwa wananitetemekea na wakanikatia tiketi za ndege… lakini nikifika nyumbani, ule u – Martha Baraka na umaarufu wangu inabidi uishie mlangoni”

Akiongea na mwanahabari wetu Yona David; Martha Baraka alionekana kumaanisha anachokisema na alikuwa na nasaha za muhimu sana kwa wasanii na waimbaji maarufu ambapo alikiri kuwa yeye kama yeye anajitahidi sana kuwa mama anapokuwa nyumbani na anamnyenyekea mume wake bila kujali kwamba jina lake ni kubwa sana kwenye jamii.




No comments:

Post a Comment