Tuesday, February 14, 2017

MJUE BENJAMIN DUBE

Mwandishi: Anderson Leng'oko

Mziki wa Afrika ya kusini ni muziki maarufu tangu kitambo. Ni mziki ambao unafahamika kwa uzuri wa melodi na tyuni zenye hisia kali sana. Kwa  upande wa muziki wa injili, Afrika Kusini imeendelea kutajwa kama nchi yenye vipaji vingi vikubwa sana.

Msanii ambaye tutamuongelea leo anaitwa Benjamin Dube. Yeye ni msanii mkubwa sana katika tasnia ya muziki wa injili wa Afrika ya kusini. Uzuri wa mashairi yake; uzuri wa nyimbo zake pamoja na nguvu ya Mungu inayopatikana katika nyimbo zake inamfanya apendwe sana.

Si hivyo tu bali Benjamini Dube anafahamika kwa unyenyekevu wake. Yeye siku zote anasema ‘in gospel we don’t have who is who, who is better than the other… but in gospel we complement each other” yaani katika mziki wainjili hatuna nani ni nani, yupi ni bora kuliko mwingine… bali katika mziki wa injili tunakamilishana.

Anafahamika kwa juhudi na kujitoa kwake katika huduma; kwani kwa mwaka anashiriki katika matoleo mawili. Anatoa toleo la kwake; anatoa toleo la Spirit of praise na anashiriki katika kuwasaidia wasanii wenzake katika matoleo yao.

Zipo nyimbo kadhaa ambazo zinaimbwa hapa Tanzania ambazo ziliimbwa naye kwa mara ya kwanza
Nazo ninakupenda eeYesu; Amen, na hakuna wa kufanana namwokozi wangu/nimemwona anapendeza.


Benjamin Dube ana watoto watatu ambao nao amewalea katika mazingira ya kuujua mziki nao wana kundi lao linaitwa the dube brothers.  Pia Benjamin Dube ana mama yake ambaye huwa anafanya naye kazi katika uimbaji.

Yeye Benjamin Dube amezaliwa katika familia ya uimbaji na yeye amehakikisha familia yake pia/watoto wake wanakuwa waimbaji na amefanikiwa sana.

Sasa hivi anatamba na toleo lake jipya linaloitwa Sanctified in His Presence lenye nyimbo kama Grateful, Bayede na Wenauyingwele. Amewashirikisha waimbaji wakubwa kama Siphokazi, Mabongi pamoja na the Dube brothers.

Pia katika toleo ambalo yeye ni mwimbaji/msanii mkuu la Spirit of Praise ambalo linatoka kila mwaka; Benjamin Dube ameimba na wasanii kadha wa kadha kama akina Omega, Tsepisho na Neyi Zimu.


Katika toleo hilo la Spirit of praise volume 6, kwa sasa anatamba na wimbo wa Lomusa Ongaka.

No comments:

Post a Comment