Mziki wa Afrika ya kusini ni muziki maarufu tangu kitambo.
Ni mziki ambao unafahamika kwa uzuri wa melodi na tyuni zenye hisia kali sana.
Kwa upande wa muziki wa injili, Afrika Kusini
imeendelea kutajwa kama nchi yenye vipaji vingi vikubwa sana.
Msanii ambaye tutamuongelea leo anaitwa Benjamin Dube. Yeye ni
msanii mkubwa sana katika tasnia ya muziki wa injili wa Afrika ya kusini. Uzuri
wa mashairi yake; uzuri wa nyimbo zake pamoja na nguvu ya Mungu inayopatikana katika
nyimbo zake inamfanya apendwe sana.
Si hivyo tu bali Benjamini Dube anafahamika
kwa unyenyekevu wake. Yeye siku zote anasema ‘in gospel we don’t have who is who,
who is better than the other… but in gospel we complement each other” yaani katika
mziki wainjili hatuna nani ni nani, yupi ni bora kuliko mwingine… bali katika mziki
wa injili tunakamilishana.
Anafahamika kwa juhudi na kujitoa kwake katika huduma; kwani
kwa mwaka anashiriki katika matoleo mawili. Anatoa toleo la kwake; anatoa toleo
la Spirit of praise na anashiriki katika kuwasaidia wasanii wenzake katika matoleo
yao.
Zipo nyimbo kadhaa ambazo zinaimbwa hapa Tanzania ambazo ziliimbwa
naye kwa mara ya kwanza
Nazo ninakupenda eeYesu; Amen, na hakuna wa kufanana namwokozi
wangu/nimemwona anapendeza.
Benjamin Dube ana watoto watatu ambao nao amewalea katika mazingira
ya kuujua mziki nao wana kundi lao linaitwa the dube brothers. Pia Benjamin Dube ana mama yake ambaye huwa anafanya
naye kazi katika uimbaji.
Yeye Benjamin Dube amezaliwa katika familia ya uimbaji na yeye
amehakikisha familia yake pia/watoto wake wanakuwa waimbaji na amefanikiwa sana.
Sasa hivi anatamba na toleo lake jipya linaloitwa Sanctified
in His Presence lenye nyimbo kama Grateful, Bayede na Wenauyingwele.
Amewashirikisha waimbaji wakubwa kama Siphokazi, Mabongi pamoja na the Dube
brothers.
Pia katika toleo ambalo yeye ni mwimbaji/msanii mkuu la
Spirit of Praise ambalo linatoka kila mwaka; Benjamin Dube ameimba na wasanii kadha
wa kadha kama akina Omega, Tsepisho na Neyi Zimu.
No comments:
Post a Comment