OUR DAILY MANA
MUNGU
MWENYE WIVU
Je, umewahi kujiuliza
ni kwa nini Mungu alikuumba? Jibu la swali hili kwa wengi linaweza kuwa kama
mtego lakini Kumbukumbu la Torati 6: 5 inasema hivi:
“Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako
wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.”
Katika maneno haya Mungu anamwuagiza mwandamu
ampende kwa moyo wote, na kwa roho yote, na kwa nguvu zote. Ukifuatilia matokeo
yanayotokea endapo mtu anafuata maagizo haya kwa uaminifu utagundua kuwa kile
Mungu anachotafuta kwa mwandamu ni KUABUDIWA.
Jinsi Mungu alivyotuumba alituumba ili tuwe
vyombo vya ibada yaani tupate kumwabudu yeye. Ndiyo maana yesu akawaambia wale
watu kuwa
“Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala; lakini ninyi
mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.” Luke 19:46
Na katika Yohana 4: 23, Yesu akasema “Lakini saa inakuja,
nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta
watu kama hao wamwabudu.”
Tunachojifunza hapa ni kuwa Mungu anafuta
watu wamwabudu katika roho na kweli. Hakuna sababu nyingine iliyomfanya Mungu
atuumbe isipokuwa ni kutaka KUABUDIWA. Ndiyo maana Musa akasema
Bwana, Mungu wako, atautahiri moyo wako, na moyo wa uzao wako, ili umpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho
yako yote, upate kuwa hai. (Deuteronomy 30:6)
Sasa swali la kujiuliza
ni nini kinatokea pale ambapo sisi tunaacha kumwabudu Mungu?
Majibu ya swali hili
yanaanzia pale Kutoka 20: 1-6
“Mungu akanena maneno haya yote akasema, Mimi ni Bwana, Mungu
wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na
miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho
chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini
chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu;
nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha
wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.”
Tunachojifunza hapa ni kuwa pale tunaposhindwa kumwabudu Mungu
katika roho na kweli, wivu wa Mungu unawaka juu yetu. Hebu chukulia mfano wa
mzazi ambaye amemtunza mwanawe vizuri na kumpa kila kitu alafu kisha mototo
huyo akaamua kuwa mkaidi na kutokumtii mzazi wake. Je, mzazi huyo atamfanyaje
mwanawe?
Mungu ni zaidi ya mzazi, ni Mungu wetu, aliyetuumba kwa sura na
mfano wake na akatuweka ili tumwabudu yeye. Ni dhahiri kuwa ni lazima Mungu awe
na gadhabu juu ya wanadamu ambao wameacha kumwabudu yeye.
Kutoka 34: 14 inasema hivi: “Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa
kuwa Bwana, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu.” Katika msitari huu Mungu
anawazuia watu wazi wazi akisema ‘hutamwabudu mungu mwingine.’
Tunaposhindwa
kumwabudu Mungu wivu wa Mungu unawake juu yetu na hiyo inamfanya Mungu
kuwapatiliza wana maasi ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne. Nahum 1:2 inasema, “Bwana
ni Mungu mwenye
wivu, naye
hujilipiza kisasi; Bwana hujilipiza kisasi, naye ni mwingi wa hasira; Bwana
hujilipiza kisasi juu ya adui zake, huwawekea adui zake akiba ya hasira.”
Wivu wa Mungu pale tunaacha kumwabudu unamfanya atunze hasira yake
katika akiba ya uharibifu. Hii inatupa kujua kuwa, ijapokuwa tunaweza kufanya
dhambi leo na kuona kana kwamba Mungu haouni, lakini jua wazi kuwa Mungu anaona
ila anakuwekea akiba ya hasira ili siku ya Mwisho iwe ni kilio na kusaga meno.
NAKUPA SHAURI MPE YESU MAISHA YAKO LEO.
YESU NI BWANA
No comments:
Post a Comment