Biblia inasema, Mungu akamwambia Ibrahim, "atakayekubariki nitambariki na atakaye kulaani nitamlaani". Kuna siri ya ajabu sana iliyofichwa ndani ya maneno haya.
Ibrahim alikuwa mtumishi wa Mungu, na kwa maana hiyo Mungu alikuwa ndani yake. Maana Biblia inasema mtakaa ndani yangu nami ndani yenu. Kwa sababu hiyo kila neno lilokuwa linasemwa juu ya Ibrahimu lilikuwa linamgusa moja kwa moja na Mungu aliyekuwa ndani yake. Kwa hiyo ukisema laana sio tu umemlaani Ibrahim bali na Mungu aliyekuwa ndani yake.
Ni muhimu sana kuwa makini na maneno unayosema juu ya watu wengine hasa watumishi wa Mungu. Kwa sababu Maneno hayo hayaendi kwa huyo mtu tu bali na kwa Mungu anayekaa ndani yake. Kwa hiyo kama ni baraka ujue kuwa umembariki Mungu na kama ni laana ujue pia kuwa unamlaani Mungu aliye ndani ya mtu huyo. Ndiyo maana biblia inasema TUMBO LA MTU LITASHIBA MANENO YA KINYWA CHAKE.
Tunamwomba Mungu wetu akusaidie tangu sasa unaposoma ujumbe huu utubu kwa sababu ya maneno uliyosema juu ya watu wengine hasa watumishi wa Mungu na uanze kujifunza kutumia kinywa chako kunena BARAKA.

No comments:
Post a Comment